BAGHDAD: Wanajeshi wanne wa Marekani wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 16.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanajeshi wanne wa Marekani wauwawa

Wanajeshi wasiopungua wanne wa Marekani waliuwawa jana katika mashambulio ya mabomu nchini Irak.

Shambulio baya zaidi lilifanywa katika wilaya ya Washia mjini Baghdad wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha alipojiripua ndani ya motokaa yake kwenye kituo cha upekuzi. Watu wanane waliuwawa katika hujuma hiyo.

Maafisa wa jeshi la Marekani wamethibitisha kuwa wanajeshi wanne wa Marekani waliuwawa na wengine wawili kujeruhiwa kwenye mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara mashariki mwa mji mkuu Baghdad.

Machafuko mapya yanayoendelea nchini Irak yanafanyika sambamba na kutolewa kwa ripoti na wizara ya ulinzi, Pentagon, inayosema mashambulio dhidi ya Wairaki na majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani yamefikia kima cha juu zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com