Baghdad. Mji wa Baghdad unaendelea na amri ya kutotembea. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Mji wa Baghdad unaendelea na amri ya kutotembea.

Sheria ya marufuku ya kutotembea mjini Baghdad inaendelea kutekelezwa kwa muda wa saa chache zijazo katika mji mkuu wa Iraq. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kutokana na sababu za serikali kuweka amri hiyo siku ya Ijumaa. Lakini kulikuwa na fununu kuwa usalama katika eneo linalolindwa sana linalojulikana kama eneo la kijani umeingia wasi wasi.

Wakati huo huo , ghasia zimeendelea katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Watu wanane wameuwawa, ikiwa ni pamoja na polisi wawili, katika mashambulizi ndani ya nje ya mji wa Baquba.

Mji huo uko kilometa 60 kaskazini ya Baghdad. Hapo mapema , mtu aliyejitoa muhanga alilenga polisi wa doria katika mji wa kaskazini wa Taj Afar, na kuuwa kiasi cha watu wawili na kuwajeruhi wengine 30.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com