1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Anis Amri

Anis Amri aliendesha gari na kuwagonga watu waliokuwa kwenye soko la Krismas mjini Berlin Desemba 2016, na kusababisha vifo vya watu 12. Siku nne baadae, alipigwa risasi na kuuawa na polisi wa Italia wakati akikimbia.

Shambulio hilo lilitukia katika eneo la Breitscheidplatz karibu na Kanisa la kumbukumbu ya Wilhem, na kusababisha vifo vya watu 12 na wengine 56 kujeruhiwa. Amri, muomba hifadhi kutoka Tunisia ambaye maombi yake yalikataliwa, alikuwa akifuatiliwa kabla ya shambulizi hilo lakini mamlaka zilishindwa kumrejesha kwao. Katika ukurasa huu unaweza kupata maudhui za DW kuhusu Anis Amri.