BAGHDAD: Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Kambi ya jeshi la Marekani yashambuliwa

Wapiganaji wa Irak waliivamia kambi ya jeshi la Marekani ya Tarmiyah, yapata kilomita 50 kaskazini mwa Baghdad hapo jana.

Uvamizi huo ulianza wakati mtu wa kujitoa mhanga maisha alipojilipua karibu na gari nje ya kambi hiyo. Baadaye wapiganaji waliingia ndani ya kambi hiyo na kukabiliana na wanajeshi wa Marekani.

Duru za jeshi la Marekani zinasema wanajeshi wawili waliuwawa na wengine 17 kujeruhiwa wakati wa uvamizi huo.

Wakaazi wanasema wanajeshi wa Marekani walipambana na wapiganaji hao baada ya mtu wa kujitoa mhanga maisha kuvuka kizuizi cha kambi hiyo. Kwa mda wa saa kadhaa helikopta zilionekana zikitua na kuondoka kutoka kambi hiyo.

Shambulio hilo lilifanywa kufuatia wimbi la mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 40 mjini Baghdad na maeneo mengine ya Irak.

Wakati huo huo, watu waliokuwa na bunduki waliwaua watu 13 waliokuwa ndani ya basi kaskazini magharibi mwa Baghdad kwa kulipinga kundi la al-qaeda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com