BAGHDAD : Iraq yataka mkakati wa pamoja dhidi ya ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 10.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Iraq yataka mkakati wa pamoja dhidi ya ugaidi

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ameyataka mataifa jirani na yale makubwa ulimwenguni kuwa na mkakati wa pamoja dhidi ya ugaidi nchini mwake.

Waziri Mkuu huyo anayepigwa vita ametaka Iraq isigeuzwe kuwa uwanja wa mapambano kati ya watu wanaowakilisha mataifa yanayohasimiana.Maliki alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja mjini Baghdad leo hii wenye lengo la kutaka kuungwa mkono kukomesha umwagaji damu wa kimadhehebu nchini humo.

Mkutano huo umewajumuisha pamoja mataifa sita jirani ya Iraq,nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wawakilishi kadhaa wa Waarabu.

Wajumbe kutoka Marekani,Iran na Syria wamepeana mikono katika mkutano huo lakini hawakuwa na mazunguzo ya pembeni.

Kulikuwa na tetesi kwamba yumkini wajumbe hao wakatumia fursa ya mkutano huo wa mataifa 16 kuwa na mazungumzo ya pande mbili juu ya masuala mbali mbali wanayohitillafiana ukiwemo mpango wa nuklea wa Iran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com