BAGHDAD: Askari zaidi wa Marekani wauawa nchini Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Askari zaidi wa Marekani wauawa nchini Iraq.

Askari saba wa Marekani wameuawa nchini Iraq kwenye miripuko ya mabomu yaliyotegwa na wanamgambo barabarani.

Kwa mujibu wa majeshi ya Marekani, askari watano miongoni mwa askari hao saba, waliuawa mjini Baghdad siku ya Alhamisi na jana.

Askari wengine wawili waliuawa siku ya Ijumaa katika jimbo la Diyala, kaskazini mwa Iraq.

Mjini Baghdad, jana, mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili yalisababisha vifo vya watu kiasi kumi na watano katika eneo la maduka yanayohudumia kwa wingi watu wa madhehebu ya Shia.

Watu kadhaa walijeruhiwa .

Wanamgambo waliovalia mavazi ya polisi pia waliwateka nyara watu wanane waliokuwa kwenye duka la mitambo ya kompyuta.

Majeshi ya Marekani yamesema yamewaua wanamgambo kumi na wanne karibu na Baghdad, kwenye eneo ambalo wanamgambo wa Kisunni wamekuwa wakikabiliana na vikosi vya serikali ya Iraq pamoja na Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com