Baa la njaa na ukame lasababisha wimbi la wakimbizi nchini Kenya | Masuala ya Jamii | DW | 11.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Baa la njaa na ukame lasababisha wimbi la wakimbizi nchini Kenya

Hali mbaya ya ukame iliyozikumba nchi za eneo la Pembe ya Afrika, pamoja pia na eneo la Kaskazini mwa Kenya, imesababisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao na kwenda kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi.

default

Wanawake na watoto wa Kisomali wakiwa katika foleni ya kupata chakula

Hali mbaya ya ukame iliyozikumba nchi za eneo la Pembe ya Afrika Ethiopia Djibouti na Somalia, pamoja pia na eneo la Kaskazini mwa Kenya imesababisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao kila siku na kwenda kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi, ambako wanaweza kupata msaada wa chakula.

Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya kwa sasa  imekuwa ikipokea wakimbizi hao wanaokimbia makaazi yao kutokana na Ukame na njaa hasa kutoka nchini Somalia.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com