ATHENS: Ubalozi wa Marekani mjini Athens washambuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS: Ubalozi wa Marekani mjini Athens washambuliwa

Mwanamke akienda sokoni Afrika Kusini

Mwanamke akienda sokoni Afrika Kusini

Mlipuko umetokea kwenye ubalozi wa Marekani mjini Athens Ugiriki kufuatia shambulio la roketi. Afisa wa polisi mjini humo amekitaja kitendo hicho kuwa cha kigaidi. Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imetangaza mjini Washinton kwamba hakuna aliyejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Magari kadhaa ya polisi yameuzunguka ubalozi wa Marekani mjini Athens na maofisa wa polisi wamezifunga barabara zote zinazoelekea eneo hilo, ikiwa ni pamoja na bustani lililo mbele ya ubalozi huo.

Vikosi vya usalama na vya kupambana na ugaidi vya Ugiriki vinalichunguza eneo la tukio. Kundi la waasi linalolitishia usalama nchini Ugiriki, liitwalo Novemba 17, ambalo zamani liliwaua wanadiplomasia wa Marekani na wa mataifa mengine ya kigeni, lilivunjwa mnamo mwaka wa 2002.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com