ANKARA: Bunge la Uturuki laidhinisha wapiga kura kumchagua rais moja kwa moja | Habari za Ulimwengu | DW | 10.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Bunge la Uturuki laidhinisha wapiga kura kumchagua rais moja kwa moja

Wabunge wa Uturuki wamepitisha mswada wa marekebisho ya katiba yanayopendekeza rais achaguliwe na wapiga kura.

Marekebisho hayo ni miongoni mwa marekebisho yaliyopangwa ya taratibu za uchaguzi.

Kwa mujibu wa spika wa bunge la Uturuki, wabunge mia tatu, sabini na sita kati ya wabunge mia tano na hamsini wameuunga mkono mswada huo ilhali wabunge hamsini na watano waliupinga.

Mapendekezo hayo yametolewa na chama tawala cha AKP kutanzua mzozo uliokuwepo bungeni kuhusu mtu anayepaswa kushikilia wadhifa wa urais.

Mapendekezo yote hayo yanapaswa kupitishwa bungeni kabla ya kuidhinishwa na Rais Ahmet Necdet.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com