ACCRA: Rais wa Ujerumani, Horst Koehler, atoa wito wa ushirkiano wa Afrika na Ulaya kwa amani ya Somalia. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA: Rais wa Ujerumani, Horst Koehler, atoa wito wa ushirkiano wa Afrika na Ulaya kwa amani ya Somalia.

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler ametoa wito kwa nchi za Afrika kushirikiana na Ulaya katika harakati za kuhakikisha amani nchini Somalia na maeneo mengine yenye mizozo barani humo.

Rais Horst Köhler alisema hayo kwenye mkutano kati yake na Rais wa Ghana, John Kuffuor mjini Accra.

Rais huyo wa Ujerumani yumo katika ziara rasmi ya siku nne nchini Ghana.

Rais John Kuffuor ameipongeza Ujerumani kwa ufadhili wa maendeleo nchini mwake.

Mwaka uliopita Ujerumani ilitoa ufadhili wa maendeleo wa zaidi ya Yuro bilioni moja kwa Ghana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com