ABUJA.Atiku Abubakar aandamwa na tuhuma za rushwa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA.Atiku Abubakar aandamwa na tuhuma za rushwa

Jopo la seneti nchini Nigeria lililoundwa kuchunguza madai ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya makamu war ais Atiku Abubakar hapo jana limeandika mashtaka rasmi dhidi yake kwa kufuja mali ya umma dollar milioni 145.

Katika ripoti yake jopo hilo limesema bwana Abubakar alitumia vibaya madaraka kwa kufuja pesa hizo ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi maalum ya nchi.

Ripoti hiyo ambayo inasubiri uamuzi wa mwisho wa bunge la Seneti imetaja kwamba sehemu ya fedha hizo zilitolewa kwa njia isiyohalali kama mikopo kwa makampuni matatu ya Network Digital Televishen NDTV, Mofas Shipping limited na Transvari Services.

Atiku Abubakar ni mgombea wa Urais wa chama cha Upinzani nchini Nigeria cha Action Congress katika uchaguzi wa Aprili mwaka huu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com