ZOMBA:Wafuasi 26 wa chama cha Upinzani wafariki ajalini Malawi | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ZOMBA:Wafuasi 26 wa chama cha Upinzani wafariki ajalini Malawi

Ajali mbaya imetokea nchini Malawi na kusababisha vifo vya wafuasi 26 wa upinzani.Ajali hiyo ya jana usiku ilitokea wakati gari la wafuasi hao wa chama cha Alliance for Demokrasi AFORD lilipopinduka.

Wafuasi hao walikuwa wakisafiri mjini Lilongwe wakitokea Blanytre kwa ajili ya kuhudhuria mkutano hii leo wa kumchagua kiongozi mpya wa chama chao kabla ya uchaguzi war ais wa mwaka 2009.

Msemaji wa polisi Franklin Gausi amewaambia waandishi wa habari kwamba wafuasi wengine 12 waliohusika kwenye ajali hiyo wako katika hali mahututi.

Polisi imesema inafanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com