1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ukomunisti

Ukomunisti ni itikadi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na vuguvugu lenye lengo kuu la kubadilisha mali binafsi na kuziweka chini ya umiliki wa umma.

Ukomunisti unaundwa kwa misingi ya umiliki wa pamoja wa njia za uzalishaji na mali asili za jamii, ili kuchukuwa nafasi ya mali binafsi na uchumi unaotegemea sekta binafsi. Mwanafalsafa na mwanidishi wa Kifaransa Victor d'Hupay aliunda neno hilo kwa maana yake ya sasa mwaka 1777, Mwingireza Thomas More pia anaelezwa kupigia chapuo aina fulani ya ukomunisti katika kitabu chake cha Utopia. Katika muundo wake wa sasa, ukomunisti ulitokana na vuguvugu la kisoshalisti la Ulaya ya karne ya 19.