1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi Jinping: China haiwezi kurudi nyuma

Sudi Mnette
1 Julai 2021

Chama cha Kikomunisti cha China leo kimeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa kuruka kwa ndege za kivita na helikopta juu na hotuba kali ya Rais Xi Jinping wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/3vqVB
China I Amsprache Präsident  Xi Jinping
Picha: Ng Han Guan/AP/picture alliance

Akizungumza kwa sauti yenye kuonesha majigambo katika moja katika hotuba kubwa ya kuadhimisha sherehe za miaka 100 ya chama tawala cha taifa lake, Chama cha Kikomunisti (CCP) huko mjini Beijing, kiongozi huyo aliuambia umma wa watu kwamba taifa hilo la Asia limeanza uelekeo wa kihistoria wa mabadiliko yasiyoweza kubadilishwa.

Amesema zile zama za China kuchinjwa na kuoneswa zimekwisha pita daima. Huku akishangiliwa kwa makofi kiongozi huyo aliendelea kwa kutoa onyo kwamba yeyote ambae atathubutu atakaejaribu kufanya hivyo dhidi ya umma wa wachina wanaopindukia bilioni 1.4 atakumbana na kizingiti kikali zaidi.

"Taifa la China ni lenye kujivunia uzalendo"

China 100. Jahrestag Kommunistische Partei | Shanghai
Gwaride la kuadhimisha miaka 100 ya CCPPicha: Aly Song/REUTERS

Zaidi kiongozi huyo mwenye nguvu amesema "Watu wa China, ni watu wanaopenda haki lakini hawaofii machafuko. Taifa la China ni taifa lenye hisia kali za kujivunia utaifa wake na kujiamini. Watu wa China hawajawahi kuonea, kudhulumu au kuwatumikisha watu wa mataifa mengine."

Aidha ameongeza kusema hawajawahi kufanya hivyo katika siku za nyumna, hawawezi kufanya sasa na wala katika siku za baadae. Katika hafla hiyo pia amekimpongeza Chama cha Kikomunisti kwa kufanikiwa kuwaondoa mamilioni ya raia swa China kutoka katika lindi la umasikini akisema watu wa China si tu wajuzi katika kuitokomeza dunia ya zamani lakini pia wapo vyema katika kuunda ulimwengu mpya.

Nia ya Tawain kurejeshwa kwenye udhibiti wa China.

Kuhusiana na suala la usalama Xi amesema taifa hilo kwa sasa linapasswa kuongeza kasi ya kufanya mageuzi ya kisasa katika ulinzi wake na jeshi. Na juu ya Taiwain anataka kufanikisha hatua ya kuungana tena na kupinga juhudi zozote za kukipa uhuru kisiwa hicho kutoka China Bara.

Tofauti na hotuba hiyo ya Rais Xi Jinping hafla hiyo ya maadhimisho ya miaka 100 Chama cha Kikomunisti cha China imefanikishwa na ushiriki wa maelfu ya waimbaji, ambao walijunga pamoja katika uwanja wa Tiananmen na kuimba nyimbo za kizalendo.

Miongoni mwa nyimbo ambayo zilizoimbwa ni pamoja na ile iliyopewa jina la "Bila ya Chama cha Kikomunisti, hakutakuwa na China Mpya." Aliyekuwa mwenyekiti wa chama na kiongozi mwenye nguvu zaidi Mao Zedong alianzisha Jamhuri ya Watu wa China mnamo 1949 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na rekodi za sasa chama hicho kinaonesha kuwa na jumla ya wanachama milioni 95 nchini China.

Vyanzo: RTR/APPE/DW