1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi Jinping alivyojilimbikizia madaraka katika muongo mmoja

Tatu Karema
11 Oktoba 2022

Muongo mmoja ulipita Xi Jinping alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama cha Kikomunisti na mwenyekiti wa baraza kuu la kijeshi wakati wa kongamano la 18 la chama hicho. Mwezi Machi mwaka uliofuata akawa rais.

https://p.dw.com/p/4I2zb
China Xi Jinping
Picha: Greg Baker/AFP/Getty Images

Katika Kongamano la 20 la Chama cha Kikomunisti nchini China, linalotarajiwa kuanza tarehe 16 Oktoba, Xi anatarajiwa pakubwa kujipatia muhula wa tatu uongozini na kudumisha hadhi yake ya mtawala mwenye nguvu zaidi nchini humo tangu Mao Zedong, mwanzilishi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Xi alijipatia mamlaka kupitia hatua maalumu alizofanya kwa wakati mmoja na nyingine hatua baada ya hatua.

Kwa kufanya hivyo alihamisha China kutoka utamaduni wa uongozi wa pamoja, ambao katibu mkuu alichukuliwa kuwa sawa na viongozi wengine katika kamati kuu ya kutunga sera ya chama cha kikomunisti hadi kwa kile ambacho sasa kinaonekana na wengi kama uongozi wa mtu mmoja.

Soma pia: Uhusiano baina ya Ujerumani na China watimiza miaka 50 ukilegalega

Kulingana na wachambuzi na wataalamu, zifuatazo ni njia kuu ambazo Xi alitumia kuimarisha utawala wake:

- Alitafuta njia ya kuchukuwa majukumu ya kutengeneza sera za kiuchumi ambayo kawaida hutekelezwa na Waziri Mkuu kwa kuongoza "vikundi vidogo vya uongozi pamoja na kundi jipya la mageuzi na fursa lililoundwa mwaka 2012 baada ya kuchukuwa mamlaka pamoja na kundi lililopo kuhusu fedha.

China Xi Jinping
Xi Jinping akiapa baada ya kuchaguliwa kwa mara ya pili wakati wa mkutano mkuu wa 13 wa chama cha Kikomunisti, Machi 17, 2018.Picha: Nicolas Asfouri/AFP/Getty Images

Alifanya kampeni kubwa ya kuwaondoa maafisa waliodhaniwa kutokuwa waaminifu, wafisadi ama kutofaa na kujenga msingi wake wa mamlaka kwa kujaza nafasi hizo zilizoachwa wazi kwa kuwateuwa washirika wake. Hadi sasa, takriban maafisa milioni 4.7  wamechunguzwa

- Xi aliwateuwa washirika wake waaminifu kusimamia masuala ya wanachama wa chama chake. Mkuu wake wa kwanza wa idara ya chama hicho alikuwa Zhao Leji, ambaye babake alifanya kazi chini ya uongozi wa babake Xi na kufuatiwa baadaye mwaka 2017 na Chen Xi aliyesoma naye katika chuo kikuu cha Tsinghua.

-Aliimarisha udhibiti wa jeshi kwa kuanzisha mageuzi makubwa na kuachisha kazi baadhi ya maafisa kutoka mwaka 2015.

-Alidhibiti vyombo vya usalama vya ndani kwa kampeni ya "usafishaji" inayoendelea ambayo iliwaondoa maafisa wakuu wengi wa idara ya polisi na majaji.

Soma pia: Xi Jinping aonya dhidi ya kuanzisha Vita vipya Baridi

- Kuanzia mwaka 2015, aliamuru bunge na taasisi nyingine ikiwa ni pamoja na baraza la mawaziri na mahakama kuu kumpa taarifa kuhusu ripoti zao za kazi za kila mwaka .

- Mnamo mwaka 2016, Xi aliliambia shirika la habari la serikali kulemea upande wa chama hicho na tangu wakati huo, uhuru wa vyombo vya habari ulipungua kwa kasi huku propaganda zinazohusiana na Xi zikiongezeka.

-Alijitambulisha rasmi kama "msingi" wa chama

China Xi Jinping
Rais Xi Jinping amejitanabahisha kama msingi wa chama cha kikomunisti cha China.Picha: Ali Haider/EPA/dpa/picture alliance

- Xi alifanyia marekebisho katiba ya chama mnamo mwaka 2017 ili kujumuisha mawazo ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye sifa za China. Kuwa na itikadi isiyojulikana kunamweka sawa na Mao na Deng Xiaoping

-Mnamo mwaka 2017, aliweka wazi jukumu kuu la chama kwa kutangaza kuwa chama hicho kinaoongoza kila kitu kutoka serikali, jeshi, watu, elimu, Mashariki, Kusini, Magharibi, Kaskazini na Kati.

Soma pia: Xi Jinping achaguliwa tena kukiongoza chama cha kikomunisti China

-Mnamo mwaka 2018 alifanya marekebisho ya katiba kufuta ukomo wa muda wa urais, na kuondoa kikwazo kwake cha kuongoza maisha.

- Katika azimio la kihistoria lililopitishwa mwaka 2021, chama hicho kiliahidi kudumisha kile kinachofahamika kama Taasisi mbili ambapo chama kinazungumza kwa uaminifu wake