1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

FDP

Kikianzishwa mnamo mwaka 1948, chama cha kiliberali kinachoelemea biashara cha FDP kimeshiriki katika serikali za Ujerumani zinazoongozwa na CDU na SPD kama mshirika mdogo kwa jumla ya miaka 45.

Chama cha FDP kinatetea biashara na uhuru binafsi, na kimekuwa kikivisaidia vyama vikubwa kuweza kutawala, baada ya vyama hivyo vya CDU na SPD kushindwa kupata wingi wa kujitosheleza kuweza kuunda serikali kivyao kwa miongo kadhaa. Mara kwa mara FDP kimejitokeza kama mshirika anaeaminika wa kuunda naye serikali. Katika uchaguzi mkuu wa 2013 kilishindwa kufikia kiwango cha asilimia 5 na hivyo kutupwa nje ya bunge, lakini kiliweza kurudi baada ya kufika na kuvuka kiwango hicho katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Onesha makala zaidi