Zimbawe yafanya marekebisho ya sheria za usalama na habari | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Zimbawe yafanya marekebisho ya sheria za usalama na habari

HARARE

Wabunge wa Zimbabwe jana wamepitisha marekebisho ya kuregeza sheria kali za usalama na vyombo vya habari nchini humo ikiwa ni hatua ya kutimiza madai ya upinzani kwa ajiili kuwa na mazingira mazuri ya kampeni kupelekea uchaguzi huru na wa haki hapo mwakani.

Televisheni ya taifa imesema kwamba marekebisho ya sheria hizo ziliopo hivi sasa kuhusu maandamano ya kisiasa na serikali kutowa leseni kwa waandishi wote yamepitishwa katika hatua ya kwanza katika bunge na wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani.

Marekebisho hayo leo yatawasilishwa kwenye baraza la juu la bunge la senate kabla ya kuwasilishwa kwa Rais Robert Mugabe kwa ajili ya kutia saini na kuwa sheria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com