1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Ukraine yahitaji msaada wa haraka kuishinda Urusi

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ukraine itashindwa katika vita vyake na Urusi iwapo bunge la Congress la Marekani halitoidhinisha msaada wa kijeshi unaohitajika kupambana na uvamizi wa Urusi

https://p.dw.com/p/4eW6P
Ukraine /Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Zelensky amesema ni muhimu kuliambia bunge hilo kwamba iwapo haitoisaidia Ukraine, basi taifa hilo litashindwa katika vita vyake na Moscow vilivyoanza miaka mitatu iliyopita.

Ameongeza kuwa itakuwa vigumu kwa raia wa ukrine kuwa hai bila ya msaada huo huku akitahadharisha kamba wakishidwa katika vita hivi hiyo inamaaniha nchi yoyote ile barani ulaya inaweza ushambuliwa na Urusi.

Mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yasababisha vifo vya watu karibu sita na 11 kujeruhiwa

Wabunge wa Repulican katika bunge hilo wamekataa kuidhinisha msaada huo hadi pale watakapopewa hakikisho pana la usalama kabla ya kuupitisha muswada wa msaada huo.