YANGON:Gambari akutana na wakuu wa utawala wa kijeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YANGON:Gambari akutana na wakuu wa utawala wa kijeshi

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchini Myanmar Ibrahim Gambari amekutana na wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kuwasilisha hisia za nchi nyingi duniani jinsi utawala wa nchi hiyo ulivyoshughulikia maandamano ya kudai demokrasia.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa alikutana na Generali Than katika mji wa Naypyitaw, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na kile walichoafikiana.

Taarifa zinasema kuwa takriban waandamanaji 200 waliuawa katika harakati za utawala huo wa kijeshi kuyazima maandamano hayo, kinyume na taarifa za serikali ya kwamba waliyouawa ni kumi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Myanmar Nyan Win akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York alisema kuwa majeshi ya usalama ya nchi hiyo yalichukua tahari wakati wa kuyazima maandamano hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com