1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Carney na Merz wazungumza pembezoni mwa mkutano wa G20

23 Novemba 2025

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz wamefanya mazungumzo kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine, hali katika Ukanda wa Gaza,

https://p.dw.com/p/544RI
Deutschland Berlin, PK Mark Carney, Friedrich Merz
Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz Picha: Tobias Schwarz/AFP/Getty Images

Viongozi hao pia wamejadili kuhusu ushirikiano katika sekta ya ulinzi, madini, nishati safi na akili mnemba.

Merz na Carney, wamekutana kando ya mkutano wa kilele wa G20, unaofanyika nchini Afrika Kusini na wamethibitisha tena uungaji mkono kwa Ukraine na kusisitiza kwamba, makubaliano yoyote ya amani ni lazima yaihusishe Kyiv moja kwa moja, yalinde maslahi yake ya msingi na yajumuishe hakikisho thabiti za usalama.

Kuhusu Gaza, viongozi hao wawili wameelezea kuunga mkono mpango jumla wa amani wenye lengo la kukomesha vita na kuwezesha misaada ya kibinadamu kuingia kwa wingi katika ardhi hiyo ya Wapalestina.