1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

G20 yasisitiza haki, amani kwenye mizozo duniani

22 Novemba 2025

Viongozi wa nchi zilizoendelea na zile zinazoinukia kiuchimi G20 wametoa wito wa "amani ya haki na ya kudumu" Ukraine, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kimabavu na Israel.

https://p.dw.com/p/543iW
Mkutano wa kilele wa G20 umefanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika Novemba, 2025
Wakuu wa nchi zilizoshiriki mkutano wa G20 Afrika Kusini Picha: Leon Neal/Getty Images

Wito huo umetolewa katika azimio la pamoja  lililotiwa saini wakati wa siku ya kwaya mkutano wa kilele wa kundi la G20 uliofunguliwa leo nchini Afrika Kusini.

Azimio hilo kati ya masuala mengilililoyagusia limesisitiza umakini katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na linasifu shauku kubwa ya kutaka kuongeza matumizi ya nishati jadidifu.

Azimio lagusia mzigo wa madeni kwa nchi masikini

Pia limezingatia mzigo mkubwa wa madeni kwa mataifa masikini. Azimio hilo limepitishwa bila mchango wowote wa Marekani hatua ambayo ikulu ya Marekani, White House imeitaja kuwa ni ya aibu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewaambia waandishi wa Habari kuwa  azimio hilo haliwezi kujadiliwa tena kauli inayoakisi mpasuko kati ya Afrika kusini na utawala wa Trump.