Waziri Mkuu al-Maliki aongoza katika uchaguzi wa Iraq | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.03.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri Mkuu al-Maliki aongoza katika uchaguzi wa Iraq

Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki, aliyesaidia kutuliza mizozo ya kimadhehebu nchini Iraq, anashika nafasi ya mbele katika uchaguzi unaotazamwa kama mtihani wa demokrasia changa nchini humo.

Iraqi Prime Minister Nuri al-Maliki speaks to supporters of Salah al- Din provinces during an election campaign rally of his list State of Law in Baghdad, Iraq on 26 February 2010. State of Law is one of the major coalitions that will take part in the March 7 parliamentary election . EPA/ALI ABBAS +++(c) dpa - Bildfunk+++

Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki akihotubia mkutano wa kampeni ya uchaguzi.

Matokeo rasmi ya mwanzo yanatazamiwa kutangazwa katika kipindi cha siku chache zijazo. Muungano wa vyama vya Kishia,"State of Law Coalition" unaoongozwa na Waziri Mkuu al-Maliki unadai kuwa upo njiani kujinyakulia ushindi katika eneo la Baghdad na katika wilaya zingine kusini mwa nchi wanakoishi Washia wengi zaidi. Hata hivyo, Nur al-Maliki anakabiliwa na changamoto kali kutoka washirika wake wa zamani wa Kishia waliounda chama cha "Iraqi National Alliance" (INA), kinachodhibitiwa na vyama viwili vikuu vya Kishia.

Wakati huo huo chama cha waziri mkuu wa zamani, Iyad Allawi, kinachotenganisha dini na siasa, kinashika nafasi ya tatu. Chama hicho kinaungwa mkono na Wairaqi wengi wa madhehebu ya Kisunni ambao ni wachache na wamepoteza ushawishi katika serikali ya al-Maliki inayodhibitiwa na Washia walio wengi.

Iraqi Prime Minister Nouri al-Mailki, left, and President Jalal Talabani, right, are seen during a meeting in Baghdad, Iraq, Friday, Oct. 17, 2008. Iraq's prime minister has acknowledged weaknesses and negatives in a draft security pact with the U.S. as Shiite and Sunni clerics complain that the government hasn't informed the public about terms of the agreement. Al-Maliki has been briefing national leaders about the draft before sending it to parliament for final approval before the U.N. mandate expires at the end the year. The deal would allow U.S. troops to remain here until at least the end of 2011 and give Iraq a role in managing U.S. military operations. (AP Photo/Khalid Mohammed)

Waziri Mkuu Nuri al-Maliki(kushoto) na Rais Jalal Talabani wa Iraq.

Na katika eneo la Wakurdi, kaskazini mwa Iraq, chama kipya kilichoundwa na mpenda mageuzi, Goran, kinashindana na chama cha PUK cha Rais Jalal Talabani. Kundi hilo jipya huenda likapunguza nguvu za PUK na KDP vilivyodhibiti katika uwanja wa kisiasa wa Wakurdi tangu miongo kadhaa. Katika siku zilizopita, mshikamano wa vyama hivyo ulisaidia kuwapa sauti Wakurdi katika siasa za Iraq.

Hivi sasa nchini Iraq, kwa sehemu kubwa, makundi yaliyokuwa yakiwakilisha jamii kwa ukabila na dini yamesambaratika. Baadhi ya makundi hayo yamevuka mipaka ya kidini na upo uwezekano wa makundi hayo kuanzisha majadiliano ya kuunda serikali mpya ya muungano, ikiwa hata chama kimoja hakitojinyakulia wingi katika bunge lenye viti 325. Majadiliano kama hayo ni mtihani kwa demokrasia dhaifu nchini Iraq, huku Marekani ikitazamia kupunguza kwa nusu idadi ya wanajeshi wake na kusitisha operesheni za kijeshi ifikapo tarehe 31 mwezi Agosti. Rais wa Marekani, Barack Obama, ameazimia kuwarejesha nyumbani wanajeshi wote wa Marekani kutoka Iraq ifikapo mwisho wa mwaka 2011.Maafisa wa Marekani wanasema mpango huo unaweza kuhatarishwa, ikiwa tu hali ya usalama itadhoofika nchini Iraq. Kwa maoni ya mtaalamu David Mack wa Taasisi ya Mashariki ya Kati, katika nchi kama Iraq haitoshi kushinda uchaguzi tu, kinachohitajiwa ni uongozi wenye ufanisi.

Mwandishi: Prema Martin/Reuters/AFP

Mhariri: Miraji Othman

 • Tarehe 08.03.2010
 • Mwandishi Prema Martin
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MMuM
 • Tarehe 08.03.2010
 • Mwandishi Prema Martin
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MMuM
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com