1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Jung aitaka Pakistan kuendelea na uchaguzi.

1 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CieF

Berlin.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amesema kuwa serikali ya Pakistan itakuwa imeshauriwa vibaya iwapo itaahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Katika mahojiano na radio moja nchini Ujerumani , Jung amesema kuwa ni muhimu kwa Pakistan kufanya uchaguzi huo kama ulivyopangwa ili kuipa nchi hiyo serikali iliyochaguliwa kidemokrasia. Kuahirisha uchaguzi , amesema , kunaweza kuleta hali mbaya nchini humo, ambayo inaweza kutumiwa na wapiganaji katika mipaka ya Pakistan na Afghanistan. Wakati huo huo ameondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi wengine zaidi wa Ujerumani wa kulinda amani nchini Afghanistan. Amesema kuwa wanajeshi 3,500 ambao tayari wako nchini humo wanatosha kuweza kufanya majukumu yote ambayo Ujerumani kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloongozwa na NATO linayafanya.