Watu wauawa katika ghasia za Naivasha Kenya | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watu wauawa katika ghasia za Naivasha Kenya

NAIROBI:

Polisi ya Kenya inasema kuwa; kwa uchache watu 19 wameuawa katika ghasia za kikabila zinazoendelea katika mkoa wa Bonde la Ufa.Mapigano kati ya kabila la rais Mwai Kibaki la WaKikuyu,dhidi ya waLuo na waKalenjin,ambao wanamuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga,yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 120 tangu Alhamisi.Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa-Koffi Annan,aliewasili nchini humo wiki jana ili kujaribu kupatanisha mgogoro wa kisiasa unaoendelea,ameziomba pande zote katika mzozo wa kisiasa ,kila moja kutaja watu wanne wa kuziwakilisha kwenye mazungumzo.Odinga anasema Kibaki aliibia kura katika uchaguzi wa rais wa Disemba 27 na anailaumu serikali kwa kuyalinda magenge ya vijana yanayofanya mashambulizi kwa raia wasio na hatia.Mapigano ambayo yalianza tangu Kibaki kutangazwa kushinda uchangauzi huo,yamesababisha watu 800 kufa na wengine robo millioni kuachwa bila makazi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com