WASHINGTON: Rais wa Afghanistan ziarani Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais wa Afghanistan ziarani Marekani

Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai ameanza ziara yake ya Marekani.Baadae leo hii na kesho Jumatatu atakutana na Rais wa Marekani,George W.Bush.Mada kuu ya mazungumzo yao inatazamiwa kuhusika na utekaji nyara wa raia 21 wa Korea ya Kusini na mhandisi wa Kijerumani,waliozuiliwa na wanamgambo wa Taliban.

Ikulu ya Washington imesema,Bush na Karzai watajadili pia masuala ya usalama na vita vya kupambana na ugaidi vinavyoongozwa na Marekani. Vile vile watachunguza upya ushirikiano wao, kuendeleza demokrasia,usalama na mafanikio ya muda mrefu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com