WASHINGTON: Rais George Bush ataupinga mswada wa pili wa kugharamia vita vya Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais George Bush ataupinga mswada wa pili wa kugharamia vita vya Iraq.

Rais wa Marekani, George W. Bush huenda akaupinga kwa kura ya turufu mswada mwingine wa kufadhili vita vya Iraq uliotayarishwa na wabunge wa chama cha Demokratic.

Msemaji wa Ikulu ya White House, Tony Snow, amesema Rais George Bush ataupinga mswada huo kwa sababu unapendekeza kufadhili kifedha vita hivyo hadi mwisho wa mwezi Julai.

Kulingana na mswada huo, bunge la Congress litakuwa na uwezo wa kusimamisha misaada iwapo hali nchini Iraq haitatengemaa.

Rais George W. Bush alikuwa ametoa wito wa dola zaidi ya bilioni tisini kugharamia vita hivyo kufikia mwezi Septemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com