WASHINGTON: Msimamo wa rais wa Sudan unasikitisha | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Msimamo wa rais wa Sudan unasikitisha

Marekani imetoa wito kwa Sudan,kuwaruhusu wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwenda Darfur.Wizara ya masuala ya kigeni ya Marekani imesema,inasikitisha sana kuwa rais Omar el-Bashir wa Sudan kwenye mkutano wa waandishi wa habari,mwishoni mwa mkutano wa kilele wa Ufaransa na Afrika,amearifu kuwa hatotoa vibali kwa tume ya wataalamu hao sita wa Umoja wa Mataifa, kuwawezesha kuingia Sudan.Hapo awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon pia aliukosoa msimamo huo wa Rais al-Bashir.Si chini ya watu 300,000 wameuawa na wengine milioni 2.5 wamelazimika kukimbia makazi yao tangu mapigano kuanza mwaka 2003 katika jimbo la Darfur,kati ya waasi na wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com