1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani yafurahishwa na uamuzi wa UM.

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgQ

Marekani imefurahishwa na azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa lililoidhinisha vikwazo dhidi ya Iran lakini imesema kuwa hatua zaidi zinahitajika kufanyika kuibinya nchi hiyo kusitisha kazi ya urutubishaji wa madini ya Urani.

Naibu waziri wa mambo ya kigeni Nicholas Burns amesema kuwa utawala wa rais Bush utajaribu kuibinya Russia, China na Japan pamoja na umoja wa Ulaya kuchukua hatua kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kusitisha kuipatia mikopo Iran.

Pia amesema Marekani inataka nchi nyingine kuacha kufanya biashara za kawaida na Iran.