WASHINGTON: Kesi za wafungwa wa Guantanamo haziwezi kusikilizwa na mahakama za majimbo | Habari za Ulimwengu | DW | 21.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Kesi za wafungwa wa Guantanamo haziwezi kusikilizwa na mahakama za majimbo

Mahakama ya Marekani imeamua kwamba wafungwa wa jela ya Guantanao Bay nchini Cuba hawawezi kuwasilisha mashtaka ya kuzuiliwa kwao katika jela hiyo kwenye mahakama za majimbo.

Mahakama ya rufaa mjini Washington imeamua kwamba mahakama hizo hazina mamlaka kusikiliza kesi za wafungwa wanaozuiliwa katika jela ya Guantanamo.

Uamuzi huo unaheshimu sheria ya tume ya jeshi iliyoidhinishwa na bunge la Congress na kutiwa saini na rais George W Bush wa Marekani mnamo mwaka jana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com