1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. George Bush kutumia kura ya veto kuzuwia kuwekwa muda wa kuondoa majeshi.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6u

Baraza la wawakilishi la Marekani limeidhinisha muswada unaotoa kiasi cha dola za Marekani bilioni 100 kwa ajili ya kuhudumia vita. Wakati huo huo , baraza hilo limeweka lengo la kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka Iraq ifikapo March 31 mwaka ujao.

Baraza hilo ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic limepitisha muswada huo kwa kura 218 dhidi ya 208.

Baraza la Seneti linatarajiwa kupiga kura kuhusiana na muswada huo leo Alhamis.

Kamanda wa majeshi ya muungano nchini Iraq David Petraeus amesema kuwa majeshi hayo yamesaidia kupunguza mauaji ya kimadhehebu katika mji wa Baghdad.

Rais George W. Bush amesema kuwa atapinga matumizi yoyote ya kijeshi kwa kura yake ya turufu iwapo yatajumuisha muda wa kuyaondoa majeshi kutoka Iraq.