WASHINGTON: Bush kuendelea na mpango wa kusikiliza kisiri zimu zinazoingia Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Bush kuendelea na mpango wa kusikiliza kisiri zimu zinazoingia Marekani

Mahakama moja ya Marekani imepitisha kwamba rais George W Bush anaweza kuendelea mbele na mpango wake wa kusikiliza kwa siri zimu zinazoingia nchini humo.

Wakati huo huo, mahakama hiyo inataka kubatilisha uamuzi wa awali uliopinga mpango huo ikiutaja kuwa uhalifu.

Rais Bush anasema mpango huo unahitajika katika vita dhidi ya ugaidi, lakini wapinzani wake wanadai unakiuka katiba katika maswala ya uhuru wa kujieleza, haki ya kutoingiliwa na uwezo wa utendaji.

Uamuzi wa mahakama hiyo unabatilisha uamuzi wa jaji wa wilaya wiki iliyopita kukataa kesi hiyo iendelee kwa muda mrefu. Kesi hiyo inatarajiwa kufika kwenye mahakama kuu ya Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com