Washambuliaji wanne wa kujitolea mhanga wapatikana na hatia Uingereza | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Washambuliaji wanne wa kujitolea mhanga wapatikana na hatia Uingereza

Washambuliaji wanne wa kujitolea mhanga wamepatikana na hatia ya kupanga njama za kutekeleza mashambulizi kwenye treni za chini kwa chini na basi, yaliyosababisha vifo vya watu 52 mwaka 2005 nchini Uingereza.

Baadhi ya watu waliojeruhiwa kufuatia shambulizi la Edgware road

Baadhi ya watu waliojeruhiwa kufuatia shambulizi la Edgware road

Hasina Patel mke wa mmoja wa washambuaji hao, katika mahojiano na runinga moja ya kimataifa nchini Uingereza amesema lilikuwa jambo la kushangaza kwake yeye baada ya kuarifiwa kuwa mumewe alikuwa mmoja wa wahusika wa mashambulizi hayo.

Mohammad Sidique Khan wa umri wa miaka 30 alilipua bomu lilokuwa kwenye mfuko ndani ya traini ya chini kwa chini katika Edgware road na kujiua papo hapo pamoja na watu wengine sita.

Kwa mujibu wa mkewe, siku mbili kabla ya kutokea kwa mashambulizi hayo Khan alikuwa amempeleka hospitalini kupokea matibabu kwani alikuwa anatajia kujifungua mtoto wa pili. Kisha baadaye alimrejesha nyumbani, na kuondoka muda mfupi baadaye akisema anakwenda kuwatembelea marafiki zake , hiyo ikawa siku yake ya mwisho kumwona tena akiwa hai.Katika wosia na barua aliyoiandika kwa mkono mlipuaji huyo alimwomba msamaha mkewe.

Polisi wa kukabiliana na ugaidi walimtia mbaroni Hasina mwezi mei kwa kumshuku huenda alishiriki katika mipango ya kupanga njama hizo za mashambulizi na kisha kumwachiliwa siku kadhaa baadaye bila mashtaka yeyote.

Taarifa nyingine ni kuwa kikao cha mwanzo cha kusikilizwa kwa kesi ya madakatari wawili walioshtakiwa kwa mashambulizi mawili ya bomu yaliyotibuka nchini uingereza mwezi mmoja uliopita kiliendelea licha ya kufeli kwa mtandao wa video katika mahakama ya jinai ya old bailey jijini london.

Daktari Bilal Abdullah wa umri wa miaka 27 kutoka iraq na Mohammed Asha wa umri wa miaka 26 kutoka jordan wanakabiliwa na shtaka la kupanga njama za kusababisha milipuko ambayo inaweza kudhuru maisha au hata kusababisha majeraha mabaya.

Maelezo kamili ya maadishi kuhusu kesi hiyo yalisambazwa kwa watetezi wote baada ya mtandao huo wa video kutoka gereza lilo na ulinzi mkali la Belmash kutoweza kupatikana. Abdullah alitiwa mbaroni baada ya shambulizi la gari ambalo halikufaulu katika uwanja wa ndege wa glasgow,scotland tarehe 30 juni.

Asha daktari katika hospitali moja kaskazini mwa Uingereza alitiwa mbaroni kufuatia msako kwenye magari punde tu ya majaribio hayo ya mashambulizi.

Mashtaka yanayomkabili Asha ni kupanga njama na Abdullah na Kafeel Ahmed ,dereva wa gari hilo lililohusika katika shambulizi ambalo halikufaulu katika uwanja wa ndege wa Glasgow tarehe 30 mwezi juni. Dereva huyo angali katika hali mahututi akiwa na majeraha mabaya ya moto.

Maafisa nchini Australia wameyaondoa mashtaka ya kuunga mkono ugaidi yaliyowasilishwa dhidi ya Mohammed Haneef. Mohammed daktari kutoka india wa umri wa miaka 27 alitiwa mbaroni kufuatia mshambulizi hayo.

 • Tarehe 27.07.2007
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2P
 • Tarehe 27.07.2007
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2P

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com