WARSAW, Mzozo wa kisiasa waikabili serikali ya Kaczynski | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WARSAW, Mzozo wa kisiasa waikabili serikali ya Kaczynski

Waziri mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski amemfuta kazi waziri wake wa mambo ya ndani.

Waziri mkuu amesema imemlazimu kuchukua hatua ya kumfurushwa kazini Janusz Kaczmarek kwasababu anatuhumiwa kuhusika na ufichuaji wa malezo muhimu na kutatiza uchunguzi juu ya madai ya rushwa katika wizara ya kilimo.Uchunguzi huo ulisababisha mwezi uliopita kufutwa kazi kwa waziri wa kilimo na naibu wake Andrzej Lepper ambaye pia anaongoza chama kimojawapo kinachounda serikali ya muungano nchini humo.

Hatua ya waziri mkuu Kaczynski imeitumbukiza zaidi Poland katika mzozo wa kisiasa na kuzusha uwezekano wa kufanyika uchaguzi wa mapema.Upande wa upinzani hapo jana ulitaka paitishwe uchaguzi wa mapema ukisema ni njia pekee iliyosalia itakayoumaliza mzozo wa kisiasa ndani ya serikali ya mseto.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com