Wanaoomba hifadhi kupata haki ya kuishi moja kwa moja nchini Ujerumani. | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wanaoomba hifadhi kupata haki ya kuishi moja kwa moja nchini Ujerumani.

Katika suala ambalo limezua mjadala mkubwa wa kisiasa nchini Ujerumani ni suala la haki za wahamiaji au wageni, na hili limetumiwa katika kuendeleza nadharia za upande wa vyama vya kihafidhina na vile vya mrengo wa shoto. Na kwa kiasi kikubwa pande hizo zimekuwa zikivutana kuhusiana na suala , la kuwashughulikia watu kiasi ya 180,000 , ambao wanaishi nchini Ujerumani, ama wale ambao hawana haki ya hadhi ya utaifa. Watu hawa wamekuwa wakipewa

hifadhi ya maridhio na kimsingi watu hawa wanaweza wakati wowote ule wakaondolewa nchini. Kuanzia leo alhamis tarehe 14 mwezi huu haki ya wahamiaji itabadilika, na kupata haki mpya ya makaazi, baada ya kupitishwa na bunge la shirikisho Bundestag, na pia baraza la wawakilishi wa majimbo, Bundesrat na ifikapo Julai mosi sheria hiyo ndio itaanza kazi rasmi.

Ujerumani inataka kuwapa idadi maalum ya watu wanaojulikana kama wenye hadhi ya maridhio , nafasi ya kupata haki ya kuishi nchini humu. Hii ni baada ya utawala wa nchi hii kuwa na majadiliano makali ya ndani baina ya vyama vya CDU/CSU na SPD.

Karibu kurasa 500 za muswada huo unaweka njia sahihi kwa ajili ya haki za wahamiaji na wanaoomba hifadhi ya kisiasa katika umoja wa Ulaya. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amekuwa mara nyingi akitetea msimamo huu, pamoja na kuingizwa katika matumizi kwa muswada huu. Mtu anapaswa pia kutambua majaribio haya ya sheria mpya ya wahamiaji na kubadilika kwa hali yao ya usalama baada ya jaribio la shambulio la bomu la sandukuni nchini Ujerumani, anaeleza waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble

Kwa jumla , na hii ndio kitu muhimu, kwa kuwa na muswada huu, maisha ya uh

usiano mwema na urafiki kwa watu ambao wanatoka katika mataifa tofauti, na wanaishi na watu wa nchi hii , yamekuwa mazuri.

Mashirika ya kuwasaidia wakimbizi kwa kweli yamefurahia sana , licha ya muda mrefu wa majadiliano kuhusu haki za watu hawa kuishi hapa. Hadi sasa haifahamiki , ni wangapi kati ya watu 180,000 ambao wanahadhi ya kuishi nchini humu kwa maridhio tu, na ambao walikuwa wanakaribia kurejeshwa makwao, ambao sasa watakuwa na haki ya kuishi moja kwa moja. Wakosoaji wanasema kuwa ni kiasi cha watu alfu kadha tu ambao watafaidika na sheria hii. Lakini muombaji ni lazima ajaze mistari kadha yenye masharti mbali mbali.

Mtu ambaye yu pekee, ni lazima awe ameishi nchini humu kwa muda wa miaka minane, na yule ambaye anafamilia itambidi awe ameishi nchini humu kwa muda wa miaka sita.

Yule ambaye ametoa taarifa ambazo si sahihi kuhusiana na maombi ya hifadhi ya kisiasa , atabaki nje ya utaratibu huu. Kutokukuhusika na mashtaka yoyote, ujuzi wa lugha ya Kijerumani na hususan kuwa na udhibitisho wa nafasi ya kazi ni mambo muhimu.

 • Tarehe 13.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHCj
 • Tarehe 13.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHCj
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com