Wanajeshi wawili wa Marekani watuhumiwa kuwauwa qairak makusudi | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wanajeshi wawili wa Marekani watuhumiwa kuwauwa qairak makusudi

Baghdad:

Uongozi wa kijeshi wa Marekani unadai kuwauwa waasi 26 katika mtaa wanakoishi washiya,katika mji mkuu wa Irak Baghdad.Waasi wengine kadhaa wamekamtwa katika mtaa wa Sadr City-Uongozi wa kijeshi wa Marekani unahoji waasi hao wana maingiliano na mtandao wa kigaidi wa Iran.Waasi waaliokamatwa Sadr City wanatuhumiwa kuingiza silaha kinyume na sheria toka Iran.Wakati huo huo jeshi la Marekani limewashitaki wanajeshi wake wawili kwa madai ya kuuwauwa makusudi wairak.Wanajeshi hao wanatuhumiwa kuwapiga risasi na kuwauwa wairak watatu kusini mwa Baghdad.Baadae wanasemekana waliweka silaha karibu na maiti hizo ili kuonyeha wamefariki kutokana na mapigano.Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa katika jela ya kijeshi nchini Kuweit wakisubiri kesi yao ifunguliwe.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com