Wanajeshi wanane zaidi wa Marekani wameuliwa nchini Irak
27 Mei 2007Matangazo
Uongozi wa kijeshi wa Marekani nchini Irak umesema wanajeshi wake wanane zaidi wameuliwa katika mashambulio tofauti yaliyojiri siku nne zilizopita nchini Irak.Shambulio baya zaidi limetokea kaskazini mwa Baghdad ambapo wanajeshi watatu wa Kimarekani waliuliwa na wawili kujeruhiwa walipokua wakipiga doria.Wengine wameuliwa ndani na pembezoni mwa mji mkuu huo wa Irak na katika mkoa wa magharibi wa Anbar.Jumla ya wanajeshi 101 wa kimarekani wameuwawa tangu may mosi iliyopita nchini Irak.