1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Marekani na Iran wafanya mazungumzo

11 Aprili 2026

Mazungumzo yameanza kati ya Marekani na Iran baada ya kufanyika majadiliano ya awali yasiyo ya moja kwa moja.

https://p.dw.com/p/5C1UG
Pakistan Islamabad 2026 | JD Vance na Shehbaz Sharif
Kushoto: Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance. Kulia: Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz SharifPicha: Pakistan's Prime Minister Office/AFP

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema anatumai Mazungumzo hayo yatasababisha kupatikana Amani ya kudumu.

Pakistan Islamabad 2026 | Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance Picha: Jacquelyn Martin/AP Photo/dpa/picture alliance

Ujumbe wa Marekani unaaoongozwa na Makamu wa Rais wa Marekani unaokutana na Iran ni kwa ajili ya kufungua njia ya kudumu ya kukomesha mapigano. Ni mkutano wa Kwanza tangu vita vilipoanza.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliosimamiwa na Pakistan yanatarajiwa kukabiliwa na vikwazo katika mazungumzo yanayoanza Jumamosi, Iran imeweka masharti kabla ya mazungumzo kuanza wakati ambapo Jeshi la Israel na wanamgambo wa Hisbollah wakiendelea kupigana kando ya mpaka wa kusini mwa Libanon.

Mapema siku ya Jumamosi Ujumbe wa Iran ulikutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif mjini Islamabad kabla ya kuanza mazungumzo na Marekani kuhusu kuvimaliza vita katika eneo the Mashariki ya Kati.

Pakistan 2025 | Muhammad Shehbaz Sharif
Waziri Mkuu wa Pakistani Muhammad Shehbaz SharifPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Iran imethibitisha kufanyika mkutano huo na imeongeza kusema kwamba maafikiano yote kati ya Iran na Marekani yatabainishwa mwishoni mwa mwa mwa mwa mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi. Amesema nchi yake imeingia kwenye mazungumzo hayo lakini haina imani na Marekani kutokana na ugeugeu wake

Kwa upande wake makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema iwapo Iran itakuwa na nia njema kwenye mazungumzo hayo basi Marekani nayo itafungua mikono yake.

Pakistan Rawalpindi 2026 | Ujumbe wa Iran ulipowasili mjini Islamabad
Kushoto: Mkuu wa majeshi wa Pakistan Jenerali Asim Munir. Wa pili Kushoto: Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi. Katikati Kulia: Spika wa Bunge la Iran Mohammad Bagher Qalibaf. Kulia: Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq DarPicha: Pakistan Ministry of Foreign Affairs/AP Photo/picture alliance

Wakati huo huo chanzo kimoja kikuu kutoka Iran kimeliambia shirika the habari la Reuters kwamba Marekani sekubali kuziachilia mali zilizofungiwa za Iran zilizokuwa zimeshikiliwa Qatar na kwenye benki zingine za kigeni. Chanzo Hicho Kimesema  Iran imekaribisha hat Hallo, Marekani. Hata hivyo Marekani imekanusha tetesi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar, Ametoa mwito kwa Marekani na Iran kushiriki wa njia ya ya kujenga katika mazungumzo mazungumzo ya Islamabad.