Wahariri wazungumzia wajibu wao wakati wa uchaguzi
5 Novemba 2007
Wahariri wa habari kutoka nchi 30 za Afrika leo wameanza mkutano wa kujadilia masuala mbalimbali yanayohusu taaluma ya uandishi.
https://p.dw.com/p/C7rN
Matangazo
Mkutano huo wa siku mbili unalenga kuzungumzia wajibu wa vyombo vya habari na maadili barani Afrika hasa wakati wa uchaguzi. Nchi ya Kenya inapanga kufanya uchaguzi tarehe 27 mwezi Disemba mwaka huu.