1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa vitabu wawalaumu viongozi wa Afrika na Ulaya

Siraj Kalyango4 Desemba 2007

Migogoro ya Zimbabwe na Darfur ni lazima ijadiliwe

https://p.dw.com/p/CWak
Vaclav Havel, rais wa zamani wa iliokuwa Czechoslovakia, sasa muandishi wa vitabu.Yeye na wenzake wawakosoa viongozi wa Afrika na UlayaPicha: AP

Migogoro ya Zimbabwe na Darfur ni lazima ijadiliwe la ladi kundi la waandishi mashuhuri wa vitabu duniani.

Kundi hilo limewalaumu viongozi wa Afrika na Ulaya kwa kushindwa kuweka katika ajenda ya mkutano wao wa kilele migogoro ya Zimbabwe na Darfur.

Mkutano huo unafanyika mwishoni mwa juma.Wandhishi hao mkiwemo ,rais wa zamani wa iliokuwa Czechoslovakia- Vaclav Havel,washindi wawili wa tuzo la nobel,Nadir Gordimer wa Afrika kusini na mwingine Gunter Grass wa Ujerumani, akiwemo Wole Soyinka wa Nigeria ,wanasema mkutano huo utakaofanyika nchini Ureno ungefaa kuwa na masuala ya Darfur na Zimbabwe katika ratiba yao ili yajadiliwe.

Viongozi kutoka Umoja wa Afrika wanakutana na wenzao wa Umoja wa Ulaya mjini Lisbon, kuanzia jumamosi hadi kesho yake,kujadilia biashara,uhamiaji na masuala mengine.

Waandhishi wa vitabu 17 kutoka Afrika na Ulaya wamewakosoa waandalizi wa mkutano huo.

Katika barua ya wazi walioitoa waandishi hao wameiita hatua ya kutoyajumuisha masuala hayo kama, uoga wa kisiasa.

Barua hiyo imetolewa na shirika lisilo la kiserikali la Crisis Action .

Kauli ya waandishi hayo ni sehemu ya migogoro inayotishia kuugubika mkutano wa Lisbon ambao Umoja wa Ulaya, unafikiri utaimarisha uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na Afrika wakati China ikiwa inanyemelea bara lililokumbwana matatizo.

Mkutano huo,wa kwanza kufanywa tangu mwaka wa 2000,umezongwa na kizungumkuti cha kumwalika kiongozi wa Zimbabwe-Robert Mugabe.Rais wa Zimbabwe analaumiwa na mataifa ya magharibi, kwa kile yanayokiita,kuvuruga uchumi wa taifa.Pia anashtumiwa kwa kuunyanyasa upande wa upinzani. Huku Waziri mkuu wa Uingereza –Gordon Brown ikiwa anatishia kususia mkutano ikiwa rais Mugabe atashiriki, waziri wa Umoja wa Ulaya anaehusika na Ureno amesema Umoja huo ni lazima umwambie Mugabe ana kwa ana kuhusu hali ya nchi yake kuliko kumzuia kushiriki.Waziri huyo,Manuel Lobo Antunes amenukuliwa kutoa mwito wa kuwepo alichokiita 'mdahalo wa kimkakati na Afrika',aliousema kuwa haujawahi kuwepo katika kanda hizo mbili.

Marekani kwa upande wake imetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe.

Waziri mdogo wa mashauri ya kigeni wa Marekani anaehusika na masuala ya Afrika-Jendayi Frazer- amesema kuwa vikwazo vya kifedha na usafiri vinalengwa watu 40 ambao ni watu wa karibu sana na Mugabe.

Katika jimbo la Darfur nchini Sudan, mgogoro wa miaka minne umesababisha watu millioni 2 kuhama makazi yao huku watu laki mbili kupoteza maisha yao.

Wanaharaki wengine wamekosoa kushiriki kwa viongozi kutoka Sudan, serikali inayolaumiwa kwa kuhusika kwa njia moja na visa vya wanamgambo wakijanjaweed,ambao wametenda maovu katika jimbo la Darfur.

Katika barua ya waandishi hao ambayo imechapishwa leo na magazeti ya Ulaya na Afrika,wamesema kuwa viongozi hao wakishindwa kujadilia masuala hayo halitakuwa jambo jema.