Vienna. Mtu mmoja ajaribu kuingia na bomu katika ubalozi wa Marekani. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vienna. Mtu mmoja ajaribu kuingia na bomu katika ubalozi wa Marekani.

Polisi wa Austria wamesema kuwa wamemkamata mtu mmoja mjini Vienna baada ya kujaribu kuingia katika ubalozi wa Marekani akiwa amebeba mfuko mgongoni uliokuwa na kile kinachoonekana kuwa bomu na misumari. Hakuna mtu aliyejeruhiwa. Vifaa vya kutambua vyuma vilifyatuka na mtu huyo , akiwa na umri wa miaka 42, mwenye asili ya Bosnia mkaazi wa mjini Vienna , alikimbia na kutupa mfuko wake mtaani karibu na ubalozi huo wakati akifukuzwa na maafisa wa polisi.

Polisi wamesema kuwa kitabu chenye maandishi ya Kiislamu kilikutwa katika nguo za mtu huyo. Wataalamu wa mabomu bado wanachunguza chombo hicho kilichokutwa katika mfuko.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com