1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yataka majibu kuhusiana na milipuko ya Nord Stream

3 Aprili 2024

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Urusi imesema imeyaandikia mataifa ya Magharibi ikiyataka yaheshimu majukumu ya kimataifa kwa ajili ya kupatikana haki, wakati wanapochunguza milipuko ya mabomba ya gesi ya Nord Stream.

https://p.dw.com/p/4eNUx
Nordstream
Mlipuko katika Bomba la gesi la NordstreamPicha: Dmytro Katkov/DW

Afisi ya mwendesha mashtaka nchini Urusi imesema imeyaandikia mataifa ya Magharibi ikiyataka yaheshimu majukumu ya kimataifa kwa ajili ya kupatikana haki, wakati wanapochunguza milipuko iliyotokea katika mabomba ya gesi ya Nord Stream na "vitendo vya kigaidi" nchini Urusi.

Mwendesha mashtaka mkuu huyo amesema wamezituma barua hizo kwa Cyprus, Ufaransa, Ujerumani na Marekani baada ya wabunge wa Urusi kuitisha taarifa kuhusu uchunguzi huo.

Urusi imeonyesha kuvunjwa moyo na uchunguzi unaoendeshwa na baadhi ya mataifa ya kigeni yenye nguvu, kuhusiana na milipuko hiyo iliyotokea Septemba 2022 katika mabomba hayo ya kusafirisha gesi ya Urusi kuelekea Ulaya magharibi.

Denmark iliacha kufanya uchunguzi Februari baada ya Sweden kuhitimisha uchunguzi wake na kuwasilisha ushahidi kwa wachunguzi wa Ujerumani.