1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yadungua makombora manne yaliyotengenezwa na Marekani

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vya ulinzi wa anga vilidungua makombora manne ya masafa marefu yaliyotengenezwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4fVlT
Kombora la masafa marefu la Marekani aina ya ATACMS
Kombora la masafa marefu la Marekani aina ya ATACMSPicha: abaca/picture alliance

Taarifa hiyo imesema makombora yaho ni baadhi ya silaha ambazo Washington imeipa Ukraine katika wiki za hivi karibuni.

Urusi imesema ndege zake za kivita na mifumo yake ya ulinzi wa anga vilidungua jumla ya makombora kumi na tano - ya aina ya ATACMS- wiki iliopita.

Afisa mmoja wa Marekani alisema mjini Washington kwamba katika wiki za hivi karibuni Marekani ilipeleka kwa siri makombora ya masafa marefu nchini Ukraine.

Afisa huyo alithibitisha kwamba makombora ya masafa ya hadi kilomita 300 kutoka Marekani yalitumika kwa mara ya kwanza mwezi Aprili kwenye Rasi ya Crimea.

Wakati huo huo, Urusi imetangaza kufungua kesi ya uhalifu dhidi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy na kumweka kwenye orodha ya watu wanaotafutwa.