1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Moto washuhudiwa Kharkiv baada ya mashambuzi ya Urusi

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Mamlaka ya mji wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine imesema moto umezuka kufuatia mashambulizi usiku kucha ya makombora na droni za Urusi.

https://p.dw.com/p/4fVG2
Wazima moto Ukraine wamesema moto mkubwa washuhudiwa Kharkiv baada ya mashambuzi ya Urusi
Wazima moto Ukraine wamesema moto mkubwa washuhudiwa Kharkiv baada ya mashambuzi ya UrusiPicha: Vyacheslav Madiyevskyy/REUTERS

Huduma ya dharura ya jimbo la Kharkiv imesema moto mkubwa zaidi uliripuka kwenye eneo la ghala na kuenea eneo la takribani umbali wa mita za mraba elfu tatu na kwamba wazima moto walipelekwa kwenye eneo hilo.

Taarifa za awali zilisema watu wanne, akiwemo mtoto, walijeruhiwa. Jeshi la anga la Ukraine linasema Urusi ilirusha droni 13 aina ya Shahed, na makombora manne aina ya S-300 na kwamba lilizidungua droni zote za Urusi.

Gavana wa jimbo la Kharkiv, Serhiy Lysak, amesema watu wengine wawili walijeruhiwa katika mashambulizi ya Urusi katika mji wa Dnipro-petro-vsk. Kwa upande wake, Urusi inasema ilidunguwa makombora manne ya masafa marefu yaliyotengenezwa na Marekani kwenye anga ya Crimea.