Umoja wa Afrika | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.02.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Umoja wa Afrika

Viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika wakubaliana juu ya kuunda mamlaka mpya itakayochukua nafasi ya tume ya sasa ya Umoja huo.

default

Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika rais Jakaya Kikwete wa Tanzania .

ADDIS ABABA.

Mkutano wa kilele wa nchi za Umoja wa Afrika unaendelea mjini Addis Ababa lakini ni viongozi 20 tu walioshiriki kwenye kikao cha kwanza kilichofanyika kwa faragha.

Habari zinasema nchi za Afrika zitaanza kutafakari njia za kuelekea kwenye kuunda serikali moja barani Afrika.

Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema viongozi kwenye mkutano huo wa Addis Ababa wamekubaliana kuunda mamlaka mpya ya Umoja wa Afrika, itakayochukua nafasi ya tume ya sasa ya Umoja huo. Akifafanua juu ya hatua hiyo, mwenyekiti wa tume hiyo Jean Ping amesema kuwa lengo la taasisi hiyo mpya ni kuunda serikali ya umoja kwa bara lote la Afrika.


 • Tarehe 02.02.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GlKr
 • Tarehe 02.02.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GlKr
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com