Umoja wa Afrika yaisimamisha uanachama Cote d′Ivoire. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Umoja wa Afrika yaisimamisha uanachama Cote d'Ivoire.

Umoja wa Afrika umeisimamisha uanachama Cote d'Ivoire, kufuatia mabishano yaliyozuka katika uchaguzi wa Rais kwenye nchi hiyo ya Afrika magharibi.

default

Rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo ambaye bado anang'ang'ania madaraka.

Afisa mmoja wa Umoja huo, amesema Cote d'Ivoire itasimamishwa uanachama mpaka pale kiongozi wa upinzani, Alassane Ouattara atakaposhika madaraka kutoka kwa mpinzani wake rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo.

Elfenbeinküste Unruhen Dezember 2010

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kikiimarisha ulinzi nchini humo.

Mpaka sasa bwana Gbagbo bado anakataa kuachia madaraka, licha ya matokeo rasmi ya uchaguzi na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kusema kwamba  mpinzani wake ameshinda uchaguzi.

Viongozi wote hao, Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara, kila mmoja anadai kushinda uchaguzi huo, hali ambayo jumuia ya kimataifa imebidi kuingilia kati.

 • Tarehe 10.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QUo5
 • Tarehe 10.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QUo5
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com