Ukumbusho wa mzingoro Berlin | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Ukumbusho wa mzingoro Berlin

Alhamis hii yatimu miaka 60 tangu Urusi kuzingiza na kufunga njia zote kwendea Berlin magharibi.

Leo imetimu miaka 60 tangu kuanzishwa safari za ndege ili kuupatia mji wa Berlin magharibi mahitaji yake -kitendo ambacho kinaangaliwa na wakaazi wa Berlin magharibi ni alama ya uhuru wao.

Katika kilele cha vita baridi kati ya kambi ya magharibi na mashariki, wanahewa wa kimarekani na Uingereza walifanya misafara ya ndege hadi 270.000 kuwasafirishia wakaazi wa Berlin magharibi hadi tani milioni 2 za chakula na mahitaji muhimu.

Mpangu huo ulikua wa kufa-kupona ili kuzuwia wakaazi hao kufa na njaa baada ya Urusi kuzifunga na kuzizingira njia zote za ardhini kwendea Berlin magharibi.

Juni,1948 kelele hizo zilikua za matumaini kwa wakaazi kiasi cha milioni 2 wa Berlin.Hatua hii ilichochewa na dola za magharibi zilizoishinda vita Ujerumani kuanzisha matumizi ya sarafu ya Ujerumani magharibi huko Berlin magharibi.

Urusi iliokua imeikalia Berlin mashariki ikajibisha kwa kufunga njia zote zilizoelekeza Berlin magharibi ikiwa za reli,magari au za majini.Shabaha ilikua kuukamua mji wa Berlin magharibi na kuulemza kabisa hadi dola za magharibi shirika zilizoshinda vita ziufute mpango wao huo .

Ulrich Kirschbau alikua mtoto mdogo wakati ule na ambae amejionea misukosuko mingi.

Mama yake alifariki dunia katika juhudi za kuwahamisha watu kuepuka maafa ya vita na akiishi na nduguye,baba yake na mama wa kambo karibu na uwanja wa Ndege wa Tempelhof.Halafu akajionea mzingiro wa Urusi.Anakumbuka:

"Nilikua mtoto wa miaka 5 na hamu yangu ilikua zaidi kucheza na marafiki zangu.Nilitambua lazima kumezuka jambo,kwavile shehena ya chakula chetu ambayo hatahivyo, haikuwa kubwa, ilizidi kupungua na wazee wangu waliingiwa na wasi wasi."

Ulrich Kirschbau ambae leo ana umri wa miaka 66 anakumbuka hata leo tena barabara nyakati zile za njaa.Mtu alifurahi na kuridhika kujipatia alao chochote cha kutafuna.Washirika wa vita vya pili vya dunia wakidondosha kutoka ndege maapul yaliokaushwa pamoja na mbatata na mboga.

Kirschbau ameeleza zaidi kwamba pale majira ya baridi yalipoingia,hali ilikua ngumu zaidi.MKuwapatia wakaazi chakula ilikua taabu zaidi kuliko hata ilivyokua miaka ya vita .Katika majira ya baridi ya mwaka 1948/49 idadi ya watu waliofariki mjini Berlin iliongezeka mno.Hata umeme ukipatikana kwa taabau .Kila mtaa ukijipatia umemed kwa masaa 2 kwa siku.

"Hii ina maana kuna wakati tukiamshwa saa 8 za usiku.Hapo taa zikirudi kuwaka na hapo watu wote huanza kutimka mbio kama vikaragosi.Watu huanza kupika,wengine kuosha na kuhamisha.Kila kitu kikifanywa kile ambacho mtu huweza anapokua na umeme.Saa hizo mbili za kujipatia umeme lazima uzitumie,kwani ikiingia saa 10 barabara alfajiri,umemeukikatwa na wakaazi wote wa Berlin magharibi wakirudi kuishi kwa kutumia ama mishumaa au vibatari endapo wakiwa na mafuta."

Kwahivyo, milio ya ndege na ndege zenyewe ilikua ni sehemu ya maisha ya Bw.Kirschbaum,alikua alilala na milio hiyo ya ndege na akiamka nayo.

Kirschbau akielewa barabara milio ya safari za ndege ilikua na maana gani -ikiashiria mema.Hata wazee walikuja kuzowea milio hiyo ya ndege ingawa milio hiyo miaka 3 hadi 4 ya nyuma ilikua na maana nyengine kabisa-vita.

Ndege zikiwaleta wakaazi wa Berlin magharibi unga wa maziwa au matunda kwenye vibati.Rubani wa kimarekani ,Gail Halvverson akiruka juu ya anga la uwanja wa ndege alidondosha kwa mwavuli mdogo kifurushi cha peremende.Watoto waliokuwa wakisubiri chini wakiokota kwa furaha.

Na hii ndio maana ndege za kimarekani zikitwa kwa utani "Madege yanayodondosha zabibu".

Pale mtoto mdogo huyu Kirschbau aliposikia chokleti zinadondoshwa huko uwanja wa ndege,alifunga safari ya huko.Lakini alipofika huko,alikuta kundi kubwa la watu:

"Nilijionea ndege tu zikiruka angani na halfu unasikia kelele za watu.Baadae unajionea kitu cheupe kikiteremka chini mitini,barabarani na hata kwenye senyenge au kwenye mapaa ya nyumba.Umati hapo unanyan'ganyia chokleti."

Ulrich Kirschbau leo ni mzee na amestaafu,lakini bado mapenzi yake ni kuwapo Uwanja wa ndege wa Tempelhof,mjini Berlin karibu na mahala alipoishi takriban sehemu kubwa ya maisha yake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com