Ujerumani yaipinga EU | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani yaipinga EU

BERLIN.Serikali ya Ujerumani umeelezea kutounga mkono mpango wa tume ya Umoja wa Ulaya wa kuweka sheria kali za kupunguza utoaji wa gesi ya carbon kutoka katika magari.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuwa sheria hiyo ni mzigo kwa Ujerumani pamoja na viwanda vyake vya magari.

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel ameuita mpango huo kuwa ni vita vya kiushindani dhidi ya viwanda vya magari vya Ujerumani na kwamba vitazinufaisha Ufaransa na Italia .viwanda vya nchi hizo vinategeza magari yasiyokuwa na nguvu kubwa.

Katika mkutano wao mjini Brussels kamati kuu ya umoja huo wa Ulaya ilipendekeza kupunguzwa kwa kiwango cha utoaji wa gesi ya Carbon kutoka katika magari mapya ya abiria.

Mapendekezo hayo yanatakiwa kuidhinishwa na nchi wanachama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com