Ujerumani ina jukumu kubwaka katika usalama wa Kosovo asema Solana | Habari za Ulimwengu | DW | 23.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani ina jukumu kubwaka katika usalama wa Kosovo asema Solana

-

BRUSSELS

Mkuu wa sera za nje wa Umaoja wa Ulaya Javier Solana amesema Ujerumani inajukumu muhimu katika kurudisha hali ya utulivu na usalama kwenye eneo la Balkan.Solana katika mahojiano na gazeti moja la hapa ujerumani la Bild am Sonntag kwamba jeshi la Ujerumani litahitajika kusaidia kuweka amani kwenye jimbo la Kosovo hadi pale wanajeshi wa jamhuri hiyo watakapokuwa tayari kuulinda usalama wa nchi yao.Ameunga mkono pia mchango uliotolewa na Ujerumani wa polisi na maafisa wa masuala ya sheria katika kusaidia ujenzi mpya wa taasisi za kiraia katika jimbo la Kosovo. Ujerumani inawanajeshi 2,200 katika jimbo hilo kama sehemu ya kikosi cha NATO.

Kwa upande mwingine Marekani imewataka maafisa wake wa kibalozi nchini Serbia kuondoka kufuatia kuzorota kwa usalama baada ya waandamanji wakiserbia kuteketeza balozi za nchi za maghabi mapema wiki hii kupinga uhuru wa jimbo la Kosovo.Waserbia katika eneo la kaskazini mwa jimbo la Kovoso pia walipambana na maafisa wa polisi wa Umoja wa mataifa wanaoweka usalama kwenye eneo hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com