Ujerumani imeahidi msaada zaidi kwa wahanga wa ukame
16 Julai 2011Matangazo
Msaada huo wa euro milioni 5, utatumiwa kuwashughulikia wakimbizi katika maeneo yaliyoathirika zaidi. Mashirika ya misaada yamekadiria kuwa kiasi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na kitisho cha njaa.
Wizara ya misaada na wizara ya mambo ya nje, zimesema kuwa msaada huo wa serikali ya Ujerumani, utagawanywa miongoni mwa mashirika ya misaada ya Ujerumani na mataifa mengine pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula-WFP.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, alitembelea Kenya jumanne iliyopita ambapo aliahidi msaada wa euro milioni 1 kwa ajili ya kambi za wakimbizi. Nusu ya msaada huo,ilitengwa kwa ajili ya matumizi ya dharura ya WFP.