Ufaransa na Italia zaungana na Uingereza kupeleka maafisa Libya | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.04.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ufaransa na Italia zaungana na Uingereza kupeleka maafisa Libya

Ufaransa na Italia zimeungana na Uingereza kupeleka maafisa wa kijeshi ili kuvisaidia vikosi vya waasi wa Libya vilivyopo eneo la mashariki.

default

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy

Ufaransa imesema inapeleka kundi la maafisa wataalamu watakaotoa ushauri wa kiufundi, mawasiliano na mipangilio mizuri.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague amesema mjini London kuwa nchi hiyo itapeleka washauri wa kijeshi 12 nchini Libya, lakini hawatahusika na kutoa mafunzo au kuwapatia silaha waasi au kusaidia shughuli za mipangilio yao.

Katika mkutano na waandishi habari, afisa mkuu wa jeshi la NATO, Admiral Russel Harding amesema jana kuwa jumuiya hiyo imewekewa mipaka na Umoja wa Mataifa ya kuwalinda tu raia.

Kommissarin der Vereinten Nationen für Menschenrechte Navi Pillay

Kamishna wa tume ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay

Wakati huo huo, mjini Geneva Kamishna wa tume ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameulaani uongozi wa Libya kwa kutumia mabomu mtawanyiko katika mji wanaouzingira wa Misrata.

Bibi Pillay, amesema kwamba mashambulio kama hayo kwenye maeneo yenye watu wengi yanaweza kuwa uhalifu wa kimataifa.

 • Tarehe 21.04.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/111bz
 • Tarehe 21.04.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/111bz
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com